Hon. Lucy Mwakyembe
MP Lucy
Mwakyembe
MP - Special Seats (CCM)
⌕

Mhe. Lucy Edward Mwakyembe Ashiriki Hafla ya Kuchangia Mfuko wa Matibabu kwa Watoto Wenye Ugonjwa wa Sikoseli

Mbunge wa Viti Maalum – Kundi la Wafanyakazi, Mhe. Lucy Edward Mwakyembe, alijumuika na viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa afya na wananchi katika hafla maalum ya kuchangia Mfuko wa Matibabu ya Upandikizaji wa Figo na Uloto kwa watoto wenye ugonjwa wa Sikoseli.

Hafla hiyo ilifanyika tarehe 16 Julai 2026 katika Ukumbi wa Mabele Mabeyo Complex, ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii na wadau mbalimbali kuchangia upatikanaji wa huduma za matibabu kwa watoto wanaoishi na ugonjwa wa Sikoseli.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa jamii katika kusaidia watoto wanaohitaji matibabu ya kibingwa ili kuboresha afya na ustawi wao.

Kwa kushiriki katika hafla hiyo, Mhe. Mwakyembe ameendelea kuonesha dhamira yake ya kuunga mkono jitihada zinazolenga kuboresha huduma za afya, hususan kwa watoto wenye mahitaji maalum ya matibabu, na kuhimiza ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuokoa maisha na kujenga taifa lenye afya bora.


Comments

Leave a Reply

Discover more from Hon. Lucy Mwakyembe MP | Official Website

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading