Hon. Lucy Mwakyembe
MP Lucy
Mwakyembe
MP - Special Seats (CCM)

Wanawake Viongozi Wahamasishe Nashat safi vijijini

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Mwakyembe ameishauri Serikali kupitia Wizara ya Nishati kufanya kampeni za kuhamasisha matumizi ya nishati safi vijijini kupitia viongozi wanawake ambapo mkakati huo utaharakisha kufikia lengo la kila mwananchi kutumia nishati hiyo.
Amesema endapo timu hiyo itaundwa kutoa elimu kata kwa
kata, itasaidia wanawake wengi waliopo vijijni ambao hawana uelewa wa matumizi ya nishati safi kupata uelewa wa kina kutoka kwa wanawake wenzao.
Aidha, amesema wao kama wanawake wa Tanzania wanamuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kuhakikisha wanawake wote wa vijijni wanaielewa nishati safi na salama na ikibidi kabla ya kufika mwaka 2034 asilimia 80 ya malengo ya Taifa iwe imepatikana.
Lucy amesema hayo leo Aprili 23, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/207.

Source: TBC online


Comments

Leave a Reply

Discover more from

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading