Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Mwakyembe amesema kuwa Kujiunga na vyama vya wafanyakazi ni hiari, na ibara ya 20 ya katiba ya Tanzania inatoa haki hiyo na sheria ya ajira na mahusiano kazini inathibitisha haki hiyo.
Baadhi ya taasisi za kazi imekuwa ikiwalazimisha wafanyakazi kwenye vyama vya wafanyakazi bila hiari yao, na baadhi ya Taasisi zina vyama zaidi ya kimoja lakini ilikuwa ni vyema kuwashauri wafanyakazi wanapoingia katika ajira Serikalini washauriwe kujiunga na vyama wanavyovihitaji.

Leave a Reply