Hon. Lucy Mwakyembe
MP Lucy
Mwakyembe
MP - Special Seats (CCM)

Mhe. Lucy Mwakyembe Akabidhi Vitenge kwa Wafanyakazi wa TTCL Zanzibar kuelekea Maadhimisho ya Mei Mosi

Mbunge wa Viti Maalum – Kundi la Wafanyakazi, Mhe. Lucy Edward Mwakyembe, Ijumaa, 24 Aprili 2026 katika TTCL Kijangwani – Zanzibar, alikabidhi vitenge kwa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Corp), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).

Katika tukio hilo, wafanyakazi walipokea vitenge hivyo kwa furaha, wakionesha mshikamano na utayari wa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya kitaifa yatakayofanyika katika Viwanja vya Dole, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Mwakyembe alisisitiza umuhimu wa kuthamini mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa, huku akiwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uzalendo.

Alieleza kuwa Maadhimisho ya Mei Mosi ni fursa muhimu ya kutambua juhudi za wafanyakazi pamoja na kuimarisha mshikamano wao, sambamba na kujadili masuala yanayohusu ustawi wao mahali pa kazi.

Aidha, alipongeza ushirikiano uliopo kati ya taasisi na wafanyakazi, akibainisha kuwa mshikamano huo ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu ya taifa.


Comments

Leave a Reply

Discover more from

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading